Mpango wa unywaji maziwa shuleni umesababisha manufaa makubwa kwa wanafunzi kuongeza uwezo wa kujifunza pamoja na kupunguza utoro shuleni.
Akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya unywaji wa maziwa shuleni duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Kilimanjaro, Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Bw. Noel Biamungu amesema kuwa mpango huo umekuwa na matokeo chanya kwani takwimu zinaonesha kupanda kwa ufaulu kwa kiasi kikubwa kwa wanafunzi wanaosoma katika shule zilizo kwenye mpango huo.
Kwa kuzingatia matokeo hayo Bw. Biamungu amewataka wadau mbalimbali hususan wazazi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa kuonesha utayari wa kuchangia gharama kidogo zinazotolewa na wazalishaji wa maziwa ili watoto waendelee kunufaika na mpango huo.
Akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye maadhimisho hayo mjini Moshi, Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira amesema zinahitajika juhudi za makusudi ili kuhakikisha kuwa mpango huo unakuwa endelevu katika shule zinazotekeleza mpoango huo sambamba na kuwashawishi wazazi na waalimu wa shule ambazo hazijanza waanze majadiliano ya mpango huo ili kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata maziwa wakiwa shuleni
Aidha Dkt. Mghwira ametoa pongezi kwa wazazi, walimu pamoja na wazalishaji mbalimbali wa bidhaa za maziwa hususan viwanda vya Nronga kilichopo wilayani hai na Fukeni wilayani Moshi kwa kufanikisha kufikisha huduma ya unywaji wa maziwa shuleni katika mkoa wa Kilimanjaro.
Mhe. Mghwira amesisitiza kuwa katika vikao vya maendeleao mkoani Kilimanjaro mpango wa unywaji maziwa shuleni lijadiliwe na kuwekewa mikakati endelevu ili idadi ya watoto wanaonufaika na mpango huo uongezeke.
Mkoa wa Kilimanjaro unatekeleza mpango wa unywaji wa maziwa shuleni kwa kuwanufaisha zaidi ya wanafunzi 7260.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa