Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imekua mstari wa mbele katika kuboresha huduma za upasuaji kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa idara ya upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya KCMC Daktari Gileard Masenga katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa utafiti wa Upasuaji salama katika bara la Afrika uliozinduliwa rasmi kitaifa katika hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro.
Dkt. Masenga amesema utafiti huo utakaofanyika kwa muda wa miaka minne unalenga kuboresha huduma za upasuaji na kusaidia kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na kukosekana kwa huduma za upasuaji katika hospitali za ngazi za chini.
Aidha ameongeza kuwa matokeo ya utafiti huo utaongeza uwezo wa madaktari kuanzia ngazi ya hospitali za wilaya kuokoa maisha ya wagonjwa kama vile majeruhi wa ajali, kinamama wajawazito na wagonjwa wengine watakaopata tiba kwa njia ya upasuaji.
Uzinduzi huo umewakuwakutanisha madaktari bingwa wa upasuaji hapa nchini na wageni kutoka katika nchi ya Zambia na Malawi.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa