Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. Kapt(Mst.) George H. Mkuchika amesma ameridhishwa na utendaji wa viongozi na watumishi waratibu wa Tasaf mkoani Kilimanjaro katika kusimamia utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf..
Mhe. Mkuchika amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi na viongozi wa mtaa wa Msaranga kata ya Msaranga Manispaa ya Moshi.
Waziri Mkuchika amesema amefanya ziara ya siku tatu katika mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kujionea utekelezaji wa mpango huo ambao unasimamiwa na wizara yake na amejionea jinsi walengwa walivyonufaishwa na mpango huo na kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wanufaika hao.
Amefafanua kuwa lengo la mradi wa Tasaf awamu ya tatu ni kuwasaidia wananchi wenye hali duni za maisha ili waweze kupata mahitaji muhimu ambayo ni chakula, mavazi na malazi lakini katika mkoa wa Kilimanjaro manufaa ya mradi huo yamenda mbali zaidi na kuwanufaisha walengwa katika nyanja zingine za maisha.
"Mimi nimefurahi sana Tasaf katika mkoa wa kilimanjaro imewezesha watoto wa walengwa kuhudhuria kiliniki, kuhudhuria shuleni wakiwa na mahitaji muhimu ikiwemo sare na viatu na familia zao kuwa na bima za afya." Amesema Waziri Mkuchika.
Aidha baadhi ya walengwa waliopata fursa ya kuzungumza na Mhe. Mkuchika wametoa shukrani zao kwa serikali kwa kuwajali na kutambua uwepo wao.
Kwa nyakati tofauti mlengwa hao wakiwemo Bibi Tedy Lyatuu na Bibi Jelenais Ngowi wamemuomba Mhe. Mkuchika awafikishie salamu zao za shukrani kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa