Serikali za mikoa ya Kilimanjaro na Manyara zimetangaza kuwa vita dhidi ya uvuvi haramu itaendelea kuwa endelevu ili kuhakikisha fursa zote zinazotokana na rasilimali zinatumika na kizazi cha sasa na kijacho.
Msimamo huo umetangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dkt. Joel Bendela katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyumba ya Mungu wilayani Simanjiro mkoani Manyara uliokuwa na lengo la kuwatangazia wananchi kufunguliwa rasmi kwa uvuvi katika bwawa la Nyumba ya Mungu..
Aidha Mhe. Bendela ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira pamaoja na Wajumbe wa Kamati za Uinzi na Usalama za Mikoa hiyo amesema kuwa hatua hiyo ni matokeo makubaliano ya pamoja ya serikali katika mikoa hiyo miwili.
Mhe. Bendera amesisitiza kuwa kufungukiwa kwa shughuli za uvuvi katika bwawa hilo nkunalenga kuwawezesha wananchi kushughulika na uvuvi halali na kupiga marufuku watu wasio waaminifu kutumia ruhusa hiyo kwa kufanya shughuli za uvuvi haramu.
Mhe. Bendela amesema mbali na ruhusa ya kufanya shughuli za uvuvi halali, wavuvi ni lazima wafuate sherea,kanuni, taratibu pamoja na masharti kadhaa yaliyowekwa na serikali ili kuhakikisha kuwa uvuvi wa samaki katika bwawa hilo unakuwa endelevu na kuleta tija kwa wananchi.
Miongoni mwa masharti ya shughuli za uvuvi ni pamoja na kuendesha shughuli zao kwa muda wa miezisita kuanzia mwezi juni hadi julai mwakani ambapo bwawa hilo litafungwa tena kwa muda wa miezi sita.
Sharti lingine ni kuhakikisha kuwa samaki watakaovuliwa wasipungue ukubwa wa nyanda tatu kwani ndiyo ukubwa sahihi unaokubalika kitaalam ili kuhakikisha kuwa samaki wachanga wanaendelea kukuwa ili watumike wakati mwingine.
Mbali na hilo wavuvu wote wametakiwa wauze samaki wao katika mialo inayokubalika na kuainishwa na serikali ili kuepuka uuzwaji wa samaki kiholela jambo ambalo litaikosesha serikali na takwimu sahihi za uvuvu na uuzaji wa samaki katika bwawa hilo.
Kuhusu usafirishaji wa samaki kutoka bwawanii kuelekea masokoni Mhe. Bendela amewataka wananchi kutumia magari yenye mabodi yenye muundo wa boksi ambayo yatakuwa na hali ya ubaridi kwa ndani inayokubaliana na uhifadhi na usafirishaji wa samaki.
Aidha serikaliza mikoa hiyo imetoa onyoatumishi wa umma na mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na dhuluma au maonyanyaso kwa wananchi wanaojisisha na shughuli za uvuvi bila kukiuka sheria na taratibu zilizowekwa.
Shughuli za uvuvi ktika bwawa la Nyumba ya Mungu zilizuiwa kuanzia Jula 1,2016 hadi Juni 30,2017 ili kuruhusu samaki kukua na kuzaliana zaidi baada ya wavuvi kuvua samaki wachanga.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa