Mwenge wa Uhuru umezindua Shule mpya ya Awali na Msingi Darajani iliyopo Kitongoji cha Faru kata ya Njiapanda kwenye Mamlaka ya Mji Mdogo wa Himo Wilayani Moshi Aprili 6, 2024.
Akizindua mradi huo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ameelekeza halmashauri kufanya maboresho madogo katika majengo ya awali ikiwemo Vyoo kwa kupandisha tofali mbili katika kuta zinazotenganisha choo kimoja na kingine vile vile eneo la nje lenye shimo ambalo amelekezeka lizibwe kwa lengo la kuepusha madhara yanayoweza kutokea kwa wanafunzi lakini kwa kushauri na kupata kibali maalumu kutoka Ofisi ya Rais - TAMISEMI.
Ndg. Mnzava amemuelekeza Mkurugenzi wa Hlamshauri ya Moshi Vijijini Shadrack M. Mhagama pamoja na Mwenyekiti Mhe. Morris Makoi kuhakikisha gata za maji zinawekwa katika majengo ya shule hiyo hata kama ziliondolewa katika maelekezo kwani itawanufaisha na uvunaji wa maji pamoja na utunzaji wa majengo hayo lakini ni vyema kutosubiri kila jambo zuri la maenendeleo kufanyiwa na Serikali.
Aidha, Ndg. Godfrey Mnzava ameendelea kusisitiza kuhusu matumizi ya Mfumo wa Manunuzi na kuhakikisha vifaa vyote vya miradi pamoja na mahitaji mengine yapitie kwenye mfumo pamoja na kuwapatia mafunzo watumishi wote waliopo chini yake kwa lengo la kukuza uelewa wa Mfumo huo.
Katika kutekeleza mradi huo, Halmashauri ilipokea fedha kiasi cha Shilingi 348,500,000.00 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kutekeleza mradi huo wenye vyumba 7 vya madarasa, jengo la Utawala, matundu 16 ya vyoo, kichomea taka, vyumba 2 vya madarasa ya awali na ununuzi wa madawati 135 na samani za ofisi.
Hata hivyo, hadi kukamilika mradi huo umetumia kiasi cha Shilingi milioni 337,771,110.98 kati ya Shilingi 348,500,000.00. Fedha zilizobaki ni Shilingi 10,728,889.02 ambazo ni fedha za matazamio.
Pia, shule hiyo imesajiliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ikipewa namba ya EM. 30205 ikiwa na idadi ya wanafunzi 377 wakiwemo wavulana 202 na wasichana 175.
Uwepo wa shule mpya hii imesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi katika darasa moja kwa kuongeza nafasi 377 za usajili wa wanafunzi, Kupunguza umbali mrefu kilomita 3 kwa wanafunzi waliokuwa wanalazimika kusoma kwenye shule zilizo mbali na makazi yao ambazo kama Shule ya Awali na Msingi Dr. Shein, Njiapanda, Himo na Korona.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa