Uzinduzi wa shule ya sekondari Ormelili
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava leo Aprili 4,1024 amezindua shule ya sekondari Ormelili Wilayani Siha yenye vyumba 8 ikiwa madarasa 2, jengo la utawala 1, maabara 3 ya sayansi ambazo ni kemia, biologia na fizikia, chumba 1 cha TEHAMA, chumba 1 cha maktaba na matundu 8 ya vyoo vya kawaida na Matundu 2 ya vyoo vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Wakati wa uzinduzi huo Ndg. Godfrey amepongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujali wananchi wa Kata ya Ormelili kwa kusogeza huduma ya Elimu karibu iliyowasaidia wanafunzi kwa kupunguza umbali wa Km. 13 wakati hapo awali walikua wakipata elimu katika shule ya jirani ya Sikirari.
Mradi huu wenye gharama ya Tshs. Milioni 588,780,029.00 ambapo nguvu za wananchi ni kiasi cha Tshs. milioni 4,500,000.00 na Serikali Kuu kupitia mradi wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (SEQUIP) 584,280,029.00 umeweza kunufaisha wananchi wa kata ya Ormelili kwa kutoa ajira zipatao 94 ikiwa wanawake 16 na wanaume 78.
Shule hiyo inauwezo wa kupokea wanafunzi 320 wa kidato cha kwanza hadi cha nne na hadi sasa ina wanafunzi 292 wa kidato cha kwanza hadi tatu.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa