Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mhe. Kapt.(Mst.) George Mkuchika amewakumbusha viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kuweka taarifa za utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini unaosimamiwa na mfuko wa maendeleo ya jamii Tassaf wanapoandaa taarifa zinazowasilishwa kwa viongozi wa kitaifa.
Waziri Mkuchika ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa za utekeezaji wa mpango wa Tassaf katika wilaya za mwanga na Same mkoani Kilimanjaro.
Mhe. Mkuchika amewataka viongozi na wananchi kukumbuka kuwa kupambana na umasikini ni moja ya ahadi za serikali kwa wananchi wakati wa kuomba ridhaa ya wananchi kuongoza nchi kupitia uchaguzi mkuu.
"Mnapowapa taarifa za maendeleo viongozi wakuu wa nchi yetu kama vile Mhe. Rais, Makamu wa Rais na Mhe. Waziri hakikisheni taarifa za Tassaf zinakuwa ni sehemu ya taarifa hizo ili wapate picha ya utekelezaji wa ahadi hii kwa wananchi" Alisema Kapt. Mkuchika.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ili kupunguza kiwango cha umaskini kwa kaya ambazo zilikuwa zinaishi chini ya mstari wa umaskini ambao walikuwa hawawezi kupata milo mitatu kwa siku.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa