Wanananchi wa Tarakea Wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wametakiwa kushiriana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa za wauzaji,wasambazaji, waingizaji na watumiaji wa dawa za kulevya.
Rai hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2018 Bw. Charles Kabeho alipozungumza na wananchi wa eneo la Tarakea wilayani Rombo.
Kabeho amesema miongoni mwa changamoto zinazoikabili serikali wilayani Rombo katika vita dhidi ya dawa za kulevya ni uwepo mpaka wa kimataifa na nchi jirani ambapo wafanyabiashara wa dawa za kulevya hutumia njia za panyaa katika kuingiza dawa za kulevya.
Kabeho amesisitiza kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya inahitaji kwa kiasi kikubwa ushiriano wa wananchi ili kuwafichua wahali hao.
Aidha Kabeho amewakumbusha wazazi kuzungumza na watoto wao kwa uwazi juu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya ili wajiepushae na matumizi ya dawa za lulevya.
Mwenge wa uhuru ulizindua clabu ya wanafunzi ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya katika eneo la tarakea.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa