Katika kuongeza ufanisi wa utendaji na kuleta maendeleo ya mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amekabidhi magari matatu kwa Wakuu wa Wilaya ya Same, Mwanga na Rombo yenye thamani ya zaidi milioni 600.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano hayo nje ya viwanja wa ofisi za Mkuu wa Mkoa, Mhe. Babu alisema serikali imeanza kutekeleza maombi mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro ya kuwapatia Wakuu wa Wilaya vitendea kazi.
Babu alisema kuwa, Wabunge wamekuwa wakilalamika Bungeni kuhusiana na wakuu wa wilaya kukosa magari ambapo mkoa ulipanga kuhakikisha bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 mpaka ifikapo mwezi Juni mwaka huu wawe wameshanunua magari matatu ya wakuu wa wilaya.
“Haya magari matatu tulipanga kuhakikisha tunayanunua mwaka huu wa fedha lakini pia tumejiwekea malengo kwa mwaka wa fedha 2024/25 tunanunua magari mengine matatu ya wakuu wa wilaya waliobakia,” alisema Babu.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa, magari hayo yatatumika kwa ajili ya shughuli za kiserikali na kuwataka kwenda kuyatunza magari hayo kwani yamenunuliwa kwa gharama kubwa.
Aliwataka kuhakikisha kuwa wakati wa sevisi yanakwenda sevisi na pia madereva kukagua gari kabla ya kuliwasha na kuondoka.
Aidha Babu amewataka Wakuu wa wilaya kuwaachia Madereva wafanye kazi zao kwani ndio waliyosomea kuendesha gari na kuachana na kumwambia kuvunja sheria ili kuwahi kule unapoenda ili kuepuka ajali zisizo na ulazima.
Nae, Mkuu wa wilaya ya Rombo, Raymond Mangwala alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wasaidizi wake na kuwapa vitendea kazi na kuahidi kutumia gari hilo kufanya kazi iliyokusudiwa ikiwemo kuhakikisha miradi inaenda kukamilika.
“Kitendea kazi hiki ambacho nimekabidhiwa namuahidi Rais nitaenda kukitumia kwa kazi zilizokusudiwa za kuwatumikia wananchi wa wilaya ya Rombo ili malengo yake yaweze kutimia” alisema Mangwala.
Aidha aliwataka viongozi wote wanaotumia magari ya umma kuheshimu sheria taratibu na kanuni za uendeshaji wa magari unaotolewa na madereva ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
“Hile ni ofsi ya dereva, hakikisha unaiheshimu kila mara na kupokea ushauri wao, tuwasikilize mara kwa mara ili kuleta matokeo chanya,
Naye Mkuu wa wilaya ya Same, Kasilda Mgeni alisema kupatikana kwa vitendea kazi kutachangia kuwafikia wananchi na kutatua kero zao .
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa