Serikali mkoani Kilimanjaro imewataka wafanyabiashara ya wa hoteli kuhakikisha wanashirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa janga la korona linadhibitiwa ili lisiingie katika mkoa wa Kilimanjaro na hatimaye nchi ya Tanzania isipate madhara makubwa kutokana na ugonjwa wa Korona.
Akiongea wakati wa kufungua mafunzo maalum ya kujikinga na kuenea kwa ugonjwa wa korona kwa wamiliki na viongozi wa hoteli katika wilaya ya Moshi, Kaimu Mkuu Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Kippi Warioba amezitaka menejimenti za hoteli wilayani Moshi kuyafanyia kazi mafunzo yaliyotolewa na wataalam wa afya mkoani ili wawe na uelewa sahihi juu maambukizi na dalili za ugonjwa wa korona.
Mhe Waariba ameleza kuwa Serikali mkoani Kilimanjaro inatekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe magufuli kwa kuhakikisha kuwa wageni wote wanaoingia nchini watawekwa chini ya uangalizi maalum kwa muda wa siku kumi na nne kabla ya kuruhusiwa kuchangamana na watu ndani ya nchi ili kuendelea na shughuli zao.
Aidha Mhe. Warioba amewaambia wafanyabiashara hao kuwa wageni watafikia katika hoteli na watakuwa chini ya usimamizi wa wataalam wa afya pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama na kuwataka wasiwe na hofu baadala yake wazingatie taratibu za kuchukua tahadhari kama zinavyotolewa na wataala wa afya na serikali ."Tusifanye mambo kwa woga na tuwe na tafsiri sahihi ili mtu asiye mgonjwa akaitwa au kuhudumiwa kama mgonjwa" alifafanua Mhe. Warioba.
Kuhusu tahadhari ya ugonjwa wa korona ndani ya hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro, Mhe. Warioba amewotoa hofu wafanyabiashara hao na wadau wote wa utallii na kuwahaikishia kuwa uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) wamejipanga kuhakikisha kuwa watu wote wako salama na endapo itatokea mgeni, muongoza wageni, mpagazi au mtumishi yeyote ataonesha dalili za ugonjwa atapata huduma na wengine kulindwa ili wasiambukizwe.
Mhe. Warioba amewataka wananchi wote kuhakikisha wananawa mikono kwa maji na sabuni mara kwa mara kwani inasaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia mtu asiambukizwe majonwa ukiwemo korona.
ili kuhakikisha kuwa kila mdau anakuwa tayari katika kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa korona Mhe. Warioba amewaagiza wafanyabiashara ya hoteli kuhakikisha wanachukua namba za simu za mkononi za wataalam wa afya ili ziwasadie kutoa taarifa endapo watapata mgeni ambaye ataonesha kuwa na dalili za ugonjwa wa korona na hatimaye serikali iweze kuchukua hatua za kunusuru maisha ya mgeni huyo na kuwalinda wananchi wengine wasiambukizwe.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa