Watanzania wametakiwa kuunga mkono hatua zinachukuliwa na serikali za kuondoa kodi, tozo na ada za kilimo, uvuvi na mifugo ambazo zinalenga kuwanufaisha watu wanajishughulisha na sekta hizo pamoja na wanaichi wote kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama .
Akifunga maonesho ya wakulima maarufu kama nanenane kwa kanda ya kaskazini yaliyofanyika jijini Arusha Mhe. Mhagama amesema lengo la serikali kuondoa tozo hizo ni kuwapunguzia mzigo wananchi ambao wamekua wakiingia gharama kulipia tozo hizo na kuwapunguzia faida katika kipato chao.
Aidha Mhe. muhagama amesisitiza kuwa itaendelea kushughulikia changamoto zote zinazoikabili sekta ya kilimo ambayo inachangia asilimia 25.5 ya ajira nchini na ni tegemeo kwa ukakika wa chakula kwa asilimia mia moja.
Waziri Mhagama amebainisha kuwa sekta ya kilimo imechangia asilimia 30.1 katika pato la taifa kwa mwaka 2017
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa