Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Kilimanjaro limekamilika kwa asilimia 93 na jumla ya wananchi walijandikisha ni milioni 1090,312.
Akizungumza na waandishiwa habari ofis kwake Mhe. Babu amesema uchaguzi wa Serikali za mitaa unafaida kubwa kwani wananchi watachagua viongozi wanaowataka watakao waletea maendeleo kwenye maeneo yao.
Hata hivyo, amewathibitishia wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro kuwa uchaguzi utakaofanyika mwezi Novemba utakuwa wa huru na haki na amewahikikishia usalama wa kila mmoja wetu kwa kuwa mkoa huu ni tulivu wakati wote.
Aidha, Mhe. Babu amewashukuru wananchi wa Mkoa huu kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura na kutoa rai kwao kujitokeza kupiga kura ifikapo Novemba 27,2024 kwani ni haki ya kila Mtanzania mwenye sifa.
Hata hivyo amesema kuwa mara baada ya kukamilika kwa taratibu za kupata wagombea kwa nafasi mbalimbali kupitia vyama vyao ratiba imebainisha kuanza kampeni za wagombea ambapo zoezi hilo litaanza tarehe 20 novemba 2024 hadi tarehe 26 novemba 2024 hivyo amewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi kusikiliza kampeni na sera za wagombea.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa