Wananchi wa wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuendelea kuiUnga mkono serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuitunza na kuitumia vema miradi ya maendeleo inayotekElezwa na serikali.
Akizumgumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa zahanati ya Kitoghoto wilayani Mwanga, kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi amesema juhudi zilizofanywa na serikali katika kuhakikisha inawaondolea wananchi adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya zinapaswa kuungwa mkono.
Awali akiwasilishs taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, mhandisi wa halmashauri ya wilaya ya mwanga Bw. Ibrahim Msangi kiasi cha cha Tsh. 119,129,048 kinatarajiwa kutumika hadi mradi utakapokamilika.
Wananchi wasiopungua 402 wanatarajia kunufaika na mradi wa zahanati ya Kitoghoto utakapokamilika.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa