Viongozi wa mila wametakiwa kurithisha watoto tamaduni , mila na desturi za makabila yalipo nchini Tanzania.
Hali hiyo itasaidia kutunza tamaduni zetu, kuzikuza na kuzitangaza kwa mataifa ya nje.
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameyabainisha hayo katika uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni lilioandaliwa na Machifu chini ya uongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo lililofanyika leo jumamosi ya tarehe 22.1.2022 kwenye viwanja vya chuo kikuu cha Ushirika.
Rais Samia ameiagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na wadau wengine kuendelea kukuza shughuli za utamaduni na mashindano ya tenzi na ushairi kwa kutumia lugha yetu ya kiswahili ili kutangaza utamaduni wa nchi kwa mataifa mbalimbali.
Aidha, Rais Samia amesema katika changamoto ya kutonyesha mvua za vuli iliyosababisha ukame na kupelekea mifugo kufa katika Halmashauri ya wilaya ya Same na Mwanga amesema serikali itakaa na wafugaji kuangalia namna bora na ya kisasa ya kupanda malisho bila kutegemea mvua.
Akiwasilisha taarifa fupi ya maendeleo ya Mkoa wa kilimanjaro Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Stephen Kagaigai amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kupatia Mkoa wa Kilimanjaro kiasi cha Tsh. Bilioni 57.39 sawa na asilimia 40% ya bajeti ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kupitia serikali ya Mkoa, Mamlaka za serikali za Mitaa, TARURA, RUWASA na TANROADS.
Mhe.Kagaigai amesema fedha hizo zimeelekezwa katika miradi ya maendeleo ikiwemo ya elimu, afya, na miundombinu ya barabara ambapo kwa upande wa elimu shule zipatazo 276 za sekondari, 18 za shule za msingi shikizi zilifanikiwa kupata fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mpambano dhidi ya UVIKO- 19 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Ameendelea kusema hivi sasa Mkoa unaendelea na maandalizi ya ujenzi wa shule mpya tisa za sekondari za Kata na ukamilishaji wa maboma 19 ya vyumba vya madarasa. Vilevile, kufuatia kuanza kwa mhula mpya wa masomo kwa mwaka 2022 Mkoa unaendelea na zoezi la uandikishaji wa watoto kwa ajili ya darasa la awali na la kwanza ambapo jumla ya wanafunzi 33,906 wa awali na wanafunzi 35,500 wa darasa la kwanza wanatarajiwa kuandikishwa.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekuli amesema wizara inafanyakazi na machifu na viongozi wa kimila ili kuendeleza na kutangaza desturi zilizo njema na kutoa elimu kwa wananchi ili kuacha mila potofu kama kukuketa, kurithi wajane na mwanamke kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi.
Amesema utamaduni ni sekta mtambuka inayotoa ajira kwa wananchi, kivutio cha utalii, kutanganza nchi pia inachangia kwenye pato la taifa.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa