Wataalam wa kilimo wilayani hai wametakiwa kuwafundisha wananchi kuongeza thamani ya mazao ili kuwawezesha kuuuza mazo kwa bei zitakazowaletea faida.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mijongweni kata ya Mnadani wilayani Hai mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira amesema wananchi wanahitaji kupewa mafunzo ya kufungasha mazao ya kilimo ili iwe rahisi kufikisha sokoni na kuuza kwa bei zitakazowanufaisha.
Aidha Mhe. Mkuu wa Mkoa amewaeleza wananchi kuwa wanapouza mazao ghafi ambayo hayajaongezwa thamani yanakuwa kwenye hatari ya kuoza kabla hajafika sokoni na hatimaye mkulima anapata hasara.
Mhe Mghira amebainisha kuwa wakulima wanapopeleka mazao nje ya nchi kabla ya kuyaongezea thamani, wanapeleka bidhaa zaidi ya moja katika zao moja na fursa za ajira nje ya nchi.
Akitolea mfano uuzaji wa mazao ya mpunga , mhe. dkt. Mghwira amesema wananchi watanufaika zaidi endapo watakoboa mpunga na kuuza mchele ambao utawawezesha kuuza kwa bei nzuri na kutumia pumba zitakazobaki kama chakula cha mifugo.
Kuhusu maendeleo ya uvuvi, Mhe. Dkt. Mghwira amewataka wataalam wa halmashauri kuwafundisha wakulima njia za kisasa za ufugaji wa samaki ili wananchi hao waweze kujikomboa kiuchumi.
Mhe. Dkt. Mghwira ameongeza kuwa endapo wananchi hususan vijana watapewa elimu ya ufugaji wa samaki itawasadia kupata ajira na hatimaye kuipunguzia serikali kazi ya kupambana na uvuvi haram katika bwawa la nyumbayamungu.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa