Wananchi wametakiwa kutowaficha watoto wenye mahitaji maalum badala yake wahakikishe watoto hao wanapata huduma zote za malezi kama watoto wengine.
Akizungumza na wananchi wa kiji cha Karansi kata ya Karansi wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kufungua jengo la madarasa mawili katika Shule ya Msingi Nuruambayo ni maalum kwa watoto wenye mahitaji maalum, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Charles Kabeho amesema kila mtoto ana haki sawa bila kujali mapungufu ya kimaumbile.
Aidha Bw. Kabeho amewataka wanajamiii kuhakikisha kuwa wanaunga mkono juhudi za watu au taasisi itakayofanya jambo lolote la kuwasadia watu wenye mahitaji maalum.
Akitoa pongezi kwa Kanisa la Kiinjiri la Kilutheri Tanzania KKKT ambao ni wamiliki wa shule ya msingi Nuru, Kabeho amewataka wananchi kuunga juhudi za kanisa hilo kwa kuchangia kwenye miundombinu na vifaa vivyoendana na hali za wanafunzi hao.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa