• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kilimanjaro Region
Kilimanjaro Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kilimanjaro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia ya Mkoa
    • Viongozi wa Mkoa
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Sekretariati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
      • Trade and Investment
      • Administration and Human Resource Department
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Teknologia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ukaguzi wa Ndani
    • Miongozo
  • Wilaya
    • Hai
    • Moshi
    • Mwanga
    • Same
    • Rombo
    • Siha
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hai
    • Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
    • Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Same
    • Halmashauri ya Wilaya ya Siha
    • Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Albam
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari

WAZIRI NDUMBARO AZINDUA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN MKOANI KILIMANJARO

Posted on: January 29th, 2025

Waziri wa Sheria na Katiba Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (MB)Nchini, amezindua kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN)  Mkoani Kilimanjaro  katika viwanja vya vumbi  vya stendi kuu ya Mabasi  Manispaa ya moshi.

Akizungumza Januari 29,2025 wakati wa uzinduzi huo amesisitiza lengo la kampeni hiyo ni kutoa elimu na msaada wa kisheria kwa wananchi wa kawaida wasio na uwezo wa kushughulikia madai yao ya kisheria kwenye maeneo yao bila gharama yoyote

Akisisitiza mambo muhimu ya kampeni hiyo amesema “katika kampeni hii yenye maudhui ya kutoa elimu itapita  Kwenye Halmashauri zote,Kata ZOTE,Vijiji vyote na vitongoji vyote pamoja na mitaa yote ili imguse kila mtanzania mwenye mahitaji hayo hivyo hakuna jiwe ambalo litaachwa bila kuguswa kila jiwe litaguswa kila migogoro litaguswa na litashughulikiwa na kutatuliwa”Amesema Ndumbaro

Aidha ametoa rai kwa baadhi ya watu wanaojificha kwenye vichaka vya uhalifu na kukiuka sheria pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu hatua kali za kisheria zitakwenda kuchukuliwa dhidi yao

“tunakwenda kuvikata hivyo vichaka na kuvichoma moto ili haki iweze kuonekana kuwa imetendeka”

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe .Nurdin Babu amewataka wananchi  kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa hiyo adhimu ili kutatua migogoro yao

“nitoe wito kwa wananchi kutumia fursa hii ya Mhe.Samia Suluh Hassan kwa mkoa wetu kujitokeza kwa wingi kuja kutoa matatizo yenu na kupata msaada wa kisheria ambao sasa unatolewa bure katika siku zote tisa mkoni hapa”Amesema Babu 

Pia Mhe.Babu  amepongeza jeshi la polisi na vyombo vya sheria mahakama  mkoani hapa kwa kuendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wananchi wanaokiuka sheria na unyanyasaji wa kijinsia

“Nalipongeza jeshi la polisi na sheria mahakama tayari tumeshafunga wananchi  wapatao 30 waliohusika na ulawiti na ubakaji wengine tumewafunga  miaka 30 na wengine kifungo cha maisha”Amesema Babu

Hata hivyo Rais wa Chama cha Wanasheria cha  Tanganyika (TANGANIKA LAWS SOCIETY) Wakili Boniface Mwambukusi ametoa wito kwa wananchi kuwa na desturi ya kuandika wosia ili kuepusha migogoro ya Ardhi na uridhi wa mali

“kwenye miradhi wosia ndio namna pekee ya wewe uliyekufa kuendelea kuzungumza na kuelekeza namna unavyotaka mali zako zisimamiwe”amesema Mwambukusi

Sambamba na hilo ameishukuru serikali kupitia wizara ya katiba na sheria kwa kutambua umuhimu wa chama cha wanasheria na mawakili kushiriki katika kutatua migogoro ya wanachi katika kampeni hiyo

Matangazo

  • Kwa Huduma Bora ya Ukumbi wa kisasa wa Mikutano, Tafadhali fika Ofisini au wasiliana nasi kwa S.L. P 3070, Moshi. au Piga simu namba 027 2758248/027 2751 February 03, 2020
  • ZOEZI LA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KUANZA MEI 16 HADI MEI 22 2025 KILIMANJARO May 15, 2025
  • MRADI WA BOOST April 01, 2023
  • Angalia Zote

Habari

  • VIJANA NA WANAWAKE MSIKOPE BILA MALENGO

    May 15, 2025
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza wananchi kumsindikiza aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, Hayati Cleopa David Msuya katika safari yake ya mwisho.

    May 13, 2025
  • Mwili wa Hayati Cleopa D. Msuya waagwa katika viwanja vya CD Msuya wilayani Mwanga

    May 12, 2025
  • SERIKALI KUTENGA BILIONI 7 KUTEKELEZA UJENZI WA BARABARA YA MABOGINI - KAHE

    May 04, 2025
  • Angalia Zote

Video

Kujisajili kwenye mfumo wa NeST - Hatua ya Awali
Video

Kiunganishi cha Haraka

  • Webmail
  • Malalamiko
  • Watumishi Portal

Tovuti zinazohusiana nasi

  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi (LIVE)
  • Mfumo wa Usambazaji Mafaili kwa njia ya Ki-Eletroniki (E-Office)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na Kufuatilia malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    17 Barabara ya Florida

    Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi

    Simu: +255 (027) 2754236/7

    Mobile:

    Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa