Viongozi katika ngazi zote mkoani Kilimanjaro watakiwa kushirikana katika kusimamia kikamilifu matumizi sahihi ya pembejeo za ruzuku inayotolewa na serikali ili ilete tija kwa wakulima na wananchi wote kwa ujumla.
Maelekezo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira katika kikao cha kamati ya ushauri ya maendeleo ya mkoa (RCC) kilichokutana tarehe 5 Machi 2021.
Mhe. Mghwira ameeleza kuwa katika msimu wa kilimo 2019/2020; mkoa wa kilimanjaro uzalisha chakula tani 1,644,008 za mazao ya chakula na biashara katika ardhi yenye ukubwa wa hekta 339,435 zilizolimwa kati ya malengo ya kuzalisha tani 1,702,160 katika hekta 353,546.
Ameongeza kuwa chakula halisi kilichozalishwa ni tani 619,426 za wanga na tani 76,165 za protini, wakati mahitaji yetu ya chakula kimkoa ni tani 453,670 za wanga na tani 45,367 za protini za mikunde.
Mhe. Dkt. Mghwira amebainisha kuwa wakulima katika mkoa wa Kilimanjaro wanaendelea na maandalizi msimu wa kilimo cha masika 2020/2021 ambao ndiyo msimu mkubwa wa kilimo kwa mwaka.
Aidha Mhe. Mghwira ametoa rai kwa viongozi na watalaamu kusimamia na kuelekeza wananchi kufanya maandalizi ya mashamba kwa wakati na kuzingatia ushauri wa kitaalamu ikiwa ni pamoja ya matumizi sahihi ya pembejeo.

Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa