Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la Msingi katika Zahanati ya Kivisini Kwanyange Wilayani Mwanga na kutoa maelekezo kwa Uongozi wa Halmashauri.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bi. Zahara Msangi kuhakikisha ifikapo Mei 20, 2024 Zahanati ya Kivisini iwe imekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mnzava ameyasema hayo leo Aprili 7, 2024 baada ya kukagua mradi huo unaoendelea na ujenzi wenye thamani ya Tshs. Milioni 90,635,407 kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo Halmashauri wamechangia kiasi cha Tshs. Milioni 38,135,407, mfuko wa jimbo Tshs. Milioni 1,600,000.00, Serikali kuu Tshs. 50,000,000.00 na nguvu za wananchi Tshs. 900,000.00 hadi kukamilika mradi huu utagharimu Tshs. Milioni 164,101,200.00.
Akisoma taarifa ya mradi kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya Dkt. Serijo Kusekwa amesema zahanati hii inaenda kuwa mkombozi kwa wananchi wa kijiji cha kwanyange na maeneo jiran wapatao 955 ambao walikua wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya hasa za baba, mama na mtoto pamoja na ushauri nasaha.
Dkt. amesema mradi huu unatekekezwa kwa utaratubu wa “force account” na kazi zinazoendelea ni kuweka sakafu, kupaka rangi, kujenga kichomeataka, shimo la kondo la nyuma na kuweka madirisha pamoja na milango.
Naye Mariamu Rashid ambaye ni wananchi wa kata ya kwa mnyange amesema zahanat hiyo itawasaidia sana kupunguza vifo vya akina mama wajawazito waliokua wakipoteza maisha njian wakati wakwenda kujifungua pamoja na watoto wachanga. Aidha, ameishukuru serikali ya awamu sita kwa kuwajali wananchi wa kata hiyo kwa kosogeza huduma za afya na huduma nyinginezo karibu. Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la Msingi katika Zahanati ya Kivisini Kwanyange Wilayani Mwanga na kutoa maelekezo kwa Uongozi wa Halmashauri.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bi. Zahara Msangi kuhakikisha ifikapo Mei 20, 2024 Zahanati ya Kivisini iwe imekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mnzava ameyasema hayo leo Aprili 7, 2024 baada ya kukagua mradi huo unaoendelea na ujenzi wenye thamani ya Tshs. Milioni 90,635,407 kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo Halmashauri wamechangia kiasi cha Tshs. Milioni 38,135,407, mfuko wa jimbo Tshs. Milioni 1,600,000.00, Serikali kuu Tshs. 50,000,000.00 na nguvu za wananchi Tshs. 900,000.00 hadi kukamilika mradi huu utagharimu Tshs. Milioni 164,101,200.00.
Akisoma taarifa ya mradi kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya Dkt. Serijo Kusekwa amesema zahanati hii inaenda kuwa mkombozi kwa wananchi wa kijiji cha kwanyange na maeneo jiran wapatao 955 ambao walikua wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya hasa za baba, mama na mtoto pamoja na ushauri nasaha.
Dkt. amesema mradi huu unatekekezwa kwa utaratubu wa “force account” na kazi zinazoendelea ni kuweka sakafu, kupaka rangi, kujenga kichomeataka, shimo la kondo la nyuma na kuweka madirisha pamoja na milango.
Naye Mariamu Rashid ambaye ni wananchi wa kata ya kwa mnyange amesema zahanat hiyo itawasaidia sana kupunguza vifo vya akina mama wajawazito waliokua wakipoteza maisha njian wakati wakwenda kujifungua pamoja na watoto wachanga. Aidha, ameishukuru serikali ya awamu sita kwa kuwajali wananchi wa kata hiyo kwa kosogeza huduma za afya na huduma nyinginezo karibu.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa